Saturday 8 August 2015

HII NI HABARI MBAYA KUTOKA MISSENYI BAADA YA KURA YA MAONI


Mwanamke mmoja,Dafrosa Severian(41) wa Kijiji Ishunju,Kata
Ishunju,Missenyi amepoteza kabisa kipande cha mdomo wake wa chini
kufuatia kung’atwa na anayemueleza kuwa ni Bi Sikitu Filemon(27) mkazi
wa kijiji hicho kufuatia ubishi juu ya matokeo ya  udiwani.

Msafiri Nyema, a,k,a Matelefoni alishinda kwa kura 477,Murshid Ibahim
kura 388 na Vicent Kamugisha kura 190.

Mwanamke huyo amefika kituo kidogo cha polisi Gera na kupewa PF3 kwa
matibabu,huku Sikitu akitafutwa


No comments:

Post a Comment