Balozi Masilingi katima moja ya majukumu |
Jioni ya Aug 11 Rais Jakaya Kikwete ametangaza
mabadiliko ya Mabalozi kadhaa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) Mabadiliko hayo yamenifikia pia mtu wangu na barua hiyo
imeandikwa hivi.
UTEUZI NA UHAMISHO WA MABALOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa
Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na
kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:
(i) Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa
Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa
Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).
(ii) Balozi Wilson Masilingi aliyekuwa Balozi wa Tanzania
nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani
kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata
Mulamula aliyeteuliwa hivi
karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa
Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico
(iii)Balozi Irene Kasyanju aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi
Wilson Masilingi.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na
uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
11 Agosti, 2015
No comments:
Post a Comment